CATHOLIC UNIVERSITY COLLEGE OF MBEYA
(CUCoM)
A Constituent College of St. Augustine University of Tanzania

"Education with virtues"

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022

Tuesday, May 25, 2021

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022

Uongozi wa CUCoM unapenda kuufahamisha umma kuwa udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2021/2022
katika ngazi ya Shahada, Astashahada na Stashahada (Bachelor Degree, Diploma & Certificate) utafunguliwa rasmi kuanzia mwezi Mei, 2021.

Kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada (Diploma & Certificate) udahili utafunguliwa kuanzia tarehe 27 Mei, 2021 na
kwa ngazi ya Shahada (Bachelor Degree), dirisha kwa wahitimu wa miaka ya nyuma (Mini-application window for graduates of previous years) litafunguliwa kuanzia tarehe 15 Juni, 2021

CUCoM inawakaribisha waombaji wote kutumia nafasi hii kutuma maombi yao ya udahili kupitia mfumo wetu wa udahili CUCoM OAS (https://oas.cucom.ac.tz). 

Kwa msaada wasiliana na ofisi ya udahili kupitia simu namba 0768 341 328 Au 0764 622 482.

Ofisi ya Udahili

CUCoM