CATHOLIC UNIVERSITY COLLEGE OF MBEYA
(CUCoM)
A Constituent College of St. Augustine University of Tanzania

"Education with virtues"

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA TATU LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022

Saturday, September 18, 2021

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA TATU LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022

Uongozi wa CUCoM unapenda kuufahamisha umma kuwa Dirisha la Tatu la udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2021/2022
katika ngazi ya Shahada (Bachelor Degree) umefunguliwa rasmi kuanzia leo tarehe 18 Septemba, 2021 Hadi tarehe 24 Septemba, 2021.

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Kwanza na ya Pili wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 18 hadi 24 Septemba, 2021 kwa namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

CUCoM inawakaribisha waombaji wote kutumia nafasi hii kutuma maombi yao ya udahili kupitia mfumo wetu wa udahili CUCoM OAS (https://oas.cucom.ac.tz). 

Kwa msaada wasiliana na ofisi ya udahili kupitia simu namba 0768 341 328 Au 0764 622 482.

Ofisi ya Udahili

CUCoM